Kocha wa Suderland, Sam Allardyce amechaguliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza akichukua nafasi ya Roy Hodgson aliyejiuzuru baada ya kufungwa dhidi ya Iceland kwenye mashindano ya Euro nchini Ufaransa.

Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo baada ya kukubaliana na Sunderland ambapo ameifundisha miezi nane na kuisadia kutoshuka daraja msimu uliopita.

Mechi ya kwanza ya kocha huyo itakuwa dhidi ya Slovakia kwenye mechi ya kufuzu kucheza mashindano ya kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Kocha huyo aliyewahi pia kuzifundisha timu za Newcastle, Blackburn na West Ham anakuwa kocha wa 15 kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *