Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye Manchester United wamekamilisha usajili wa kiungo wa Juventus, Paul Pogba kwa ada ya uamisho iliyovunja rekodi paundi milioni 89.

Kiungo huyo wa ufaransa amepimwa vipimo vya afya katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo Carrington na kusaini mkataba wa miaka mitano ndani ya Manchester United.

PG

Paul Poga aliondoka Manchester United na kujinga na Juventus mwaka 2012 baada ya kukosa namba ya kudumu chini ya aliyekuwa kocha wa wakati huo, Sir Alex Ferguson ambapo alimuachia huru kuondoka na kujinga na mabingwa hao wa Italia.

Pogba ni miongoni mwa wachezaji waliyeisaidia Ufaransa kutinga fainali ya mashindano ya Euro ambapo walifungwa dhidi ya Ureno kwenye fainali hiyo.

Hadi sasa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameshasajili wachezaji wanne wapya kwenye kikosi hicho ambao ni Zlatan Ibrahimovic kutoka PSG, Eric Bailly kutoka Villereal, Enrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund na Paul Poga kutoka Juventus.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *