Mshambuliaji wa zamani wa Taifa Stars, Mrisho Ngassa amejiunga na Mbeaya City kutokea klabu ya Fanja FC ya Oman baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Ngassa amesaini wino kuitumikia klabu ya Mbeya City fc akiungana na nyota wengine 9 waliojumishwa kikosini kwenye usajili wa dirisha dogo lililofikia tamati desemba 15.

Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja utaomuweka kwenye kikosi cha Kinnah Phiri mpaka Novemba 30, 2018,na kukabidhiwa jezi namba 10.

Baada ya kusaini mkataba huo wa mwaka mmoja Ngassa amesema anatakakufanya kazi kwa kiwango ambacho kitaipa mafanikio timu yake mpya na kuwaziba ‘midomo’ wale wanaamini kwamba soka lake limefikia tamati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *