Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva amejiunga na klabu ya Difaa Hassani El Jadidi ya Morocco kwa mkataba wa miaka mitatu.

Msuva ambaye aliisadia timu ya Yanga kushinda kombe la ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo.

Timu ya  Difaa Al Jadid ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Morocco na timu hiyo itashiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Africa msimu ujao.

Msuva aliondoka Dar es Salaam Julai 26, 2017 kwenda Morocco kukamilisha taratibu za usajili huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *