Borussia Dortmund imemsajili kiungo wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich, Mario Gotze kwa mkataba wa miaka minne kwa dau la Paundi Milioni 22.

 

Gotze amejiunga na Bayern Munich mwaka 2013 akitokea klabu ya Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 32 amesaini mkataba wa miaka minne ambao utamuweka mpaka mwaka 2020 na atakamilisha uhamisho wake baada ya vipimo vya afya.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake na Bayern Munich lakini anaondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuambiwa kama hayupo kwenye mipango ya kocha Carlo Ancelotti.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *