Baraza la Wadhamini wa Yanga SC limeikabidhi timu kwa kampuni ya Yanga Yetu, inayomilikiwa na Mwenyekiti wake, Yussuf Manji ambayo itakuwa mmiliki wa klabu kwa miaka 10.

Agosti 6 mwaka huu wanachama wa Yanga walikubali kumkodisha klabu hiyo kiongozi wao huyo mkuu kwa miaka 10 na tangu hapo taratibu zimekuwa zikiendelea kimyakimya hadi mapango huo umekamilika.

Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu wa dharula uliofanyika Agosti 6, ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es Salaam.

Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.

Katika kipindi hicho cha miaka 10 timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini yake Manji.

Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu, Francis Kifukwe amesema baada ya wanachama kuridhia mpango huo wao wanampa pia ridhaa hiyo Manji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *