Kocha wa zamani wa Manchester United na Uholanzi, Louis van Gaal amestaafu kufundisha soka baada ya kufanya kazi hiyo kwa kipindi cha miaka 26.

Van Gaal mwenye umri wa miaka 65 alikuwa nje ya kazi hiyo toka afukuzwe kwenye klabu ya Manchester United masaa machache baada ya kushinda kombe la FA.

Kocha huyo amesema kuwa anafikiria muda wa kupumzika kufundisha soka umefika kwasasa baada ya kufundisha kwa kipindi cha miaka 26 kwenye timu tofauti.

Kocha huyo amesema hayo wakati akipewa tuzo ya mafanikio na Serikali ya Uholanzi kutokana na mchango wake katika mpira wa miguu.

Timu alizofundisha Van Gaal na mafanikio yake

 

Mataji ya Ligi kuu : Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96), Barcelona (1997-98, 1998-99), AZ Alkmaar (2008-09), Bayern Munich (2009-10)

Klabu Bingwa Ulaya: Ajax (1994-95)
Kombe la Uefa: Ajax (1991-92)
Kombe la FA: Manchester United (2015-16)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *