Manchester City wamekamilisha usajili wa beki wa kulia wa Tottenham na England Kyle Walker kwa dau la paundi milioni 45.

Walker, ambaye amechezea taifa lake mechi 27 na amekuwa na Spurs kwa msiimu minane, ametia saini mkataba wa miaka mitano City.

Uhamisho wake, ambao unakuwa na jumla ya £50m ukiongeza kikolezo cha £5m, huenda ukamfanya kuwa mchezaji ghali zaidi wa England kuwahi kuwepo.

Walker alijiunga na Spurs kutoka Sheffield United mwaka 2009 na amecheza mechi 183 Ligi ya Premia.

Mchezaji huyo anataraji kusafiri na City siku ya Jumatatu kwa ziara yao ya Marekani na atavaa jezi namba mbili.

Wachezaji ghali zaidi wa Uingereza

£85.3m – Gareth Bale (Tottenham kwenda Real Madrid, 2013)
£49m – Raheem Sterling (Liverpool kwenda Manchester City, 2015)
£47.5m – John Stones (Everton kwenda Manchester City 2016)
£45m – Kyle Walker (Tottenham kwenda Manchester City 2017)

£35m – Andy Carroll (Newcastle kwenda Liverpool, 2011)

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *