Paris St-Germain wamemsajili mshambuliaji wa Uispania, Jese Rodriguez kutoka Real Madrid ambapo ada ya uamisho aijawekwa wazi lakini amesaini mkataba wa miaka mitano kuwatumikia mabingwa hao wa Ufaransa.

Jese mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Real Mdrid akiwa na umri wa miaka 14 na alikuwa miongoni mwa wachezaji walioshinda ubingwa wa Ulaya mara mbili akiwa na Real Madrid mwaka 2014 na 2016.

 Kiwango chake kimemvutia kocha wa zamani wa Sevilla, Unai Emery ambaye amechukua nafasi ya kocha wa zamani wa PSG Laurent Blanc kuwanoa mabingwa hao wa Ufaransa.

Baada ya kusaini Jese amesema kwamba anajisikia vizuri kusajiliwa na PSG kwani ni timu kubwa na ina kocha mwenye uzoefu na ana amini atafanya vizuri ndani ya kikosi hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *