Klabu ya Manchester City imekamilisha usajili wa golikipa Claudio Bravo kutoka Barcelona.

Golikipa huyo raia wa Chile mwenye umri wa miaka 33 anatarajiwa kuanza kwenye kikosi hiko nyuma ya golikipa wa Uingereza, Joe Hart na muargentina, Willy Caballero.

Barcelona tayari wameshamsajili golikipa wa Uholanzi, Jasper Cillessen kutoka klabu ya Ajax.

Bravo alijiunga na Barcelona mwaka 2014 na ameshinda mataji mawili ya La Liga na moja la klabu bingwa barani Ulaya na kombe la klabu bingwa dunia.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *