Winga wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Yannick Bolasie amejiunga na Everton kwa dau la paundi milioni 28 akitokea Crystal Palace.

Balasie amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu hiyo ya Goodson park mpaka msimu wa mwaka 2021.

Baada ya kusaini mkataba huo Balassie amesema kwamba amefurahishwa kujiunga na klabu ya Everton kwani ni klabu kubwa na anamatumaini ya kufanya vizuri chini ya kocha mpya Ronald Koeman.

Bolassie aliingia kipindi cha pili kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ambapo timu yake ya hapo awali Crystal Palace ilipofungwa dhidi ya Westbromwich katika uwanja wa nyumbani.

Kwa upande wa kocha wa Everton, Ronald Koeman amesema kwamba amemnunua mchezaji huyo kwasababu ana uwezo mkubwa wa kusakata kandanda kwahiyo anamatumaini atacheza kwa mafanikio na timu yake hiyo mpya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *