Klabu ya Borussia Dortmund imemsajili winga wa kimataifa wa Ujerumani, Andera Schurrle kutoka timu ya Wolfsburg ambapo dau la uhamisho huo ujawekwa bayana.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano na timu hiyo yenye maskani yake Westfalenstadion nchini Ujerumani.

Schurrle ameshinda magoli 48 kwenye mechi 174 katika ligi ya Bundesliga na goli 20 akiifungia timu yake ya taifa katika mechezo 55 na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichofika hatua ya nusu fainali kwenye mashindano ya Euro nchini Ufaransa.

Kiungo huyo alijiunga na Wolfsburg akitokea Chelsea mwezi Februari mwaka 2015 kwa dau la paundi milioni 22.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *