Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford amefunga magoli matatu baada ya timu yake ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 kuifunga Norway 6-1 kwenye mechi ya kufuzu kombe ka Ulaya.

Mshambuliaji huyo ameshinda goli hizo baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi hiyo iliyofanyika jana nchini Uingereza.

Marcus ni mshambuliaji hatari kwasasa kutokana na kuonesha kiwango cha hali ya juu kadri siku zinavyokwenda mpaka kupelekea gwiji wa soka duniani Pelle kukuibali kiwango cha mshambuliaji huyo.

rashd

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce aliamua kumpeleka mshambuliaji huyo kwenye kikosi cha chini ya Umri wa miaka 21 kutokana na kukosa namba ya kudumu katika timu yake ya Manchester United chini ya Jose Mourinho.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Uingereza chini ya umri wa miaka 21 walikuwa wanaongoza goli 2-0 na mpaka mpira uanamalizika Uingereza imeshinda 6-1 dhidi ya Norway.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *