Manchester United imeingiza mguu mmoja fainali baada kushinda 1-0 dhidi ya Celta Vigo katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Euefa Europa Ligi.

Goli pekee la Manchester United limewekwa kimiani na mshambuliaji, Marcus Rashford mnamo dakika ya 67 kipindi cha pili cha mchezo.

Timu hizo zitarejeana tena Alhamisi wiki ijayo katika dimba la Old Trafford jijini Manchester nchini Ungereza.

Wachezaji wa Manchester United wakishangilia goli dhidi ya Celta Vigo
Wachezaji wa Manchester United wakishangilia goli dhidi ya Celta Vigo

Baada ya mchezo huo Timu hizo zitarejeana tena Alhamisi wiki ijayo huko Old Trafford Maskani ya Manchester United.

Kwa upande wa Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa kijana huyo ni mdogo kwa kwa maana ya umri wa miaka 19, mi kijana ambaye anapenda mpira, kila akimaliza mazoezi na wenzake anabaki uwanjani kwa dakika 30 kupiga free-kicks kila siku ili kujinoa zaidi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *