Kocha wa timu ya taifa ya Wales, Chris Coleman amesema majeruhi ya misuli ya paja aliyopata mchezaji wake Aaron Ramsey yatamfanya akose mechi ya kwanza ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Moldova itakayofanyika Septemba 5 mwaka huu.

Ramsey alipata majeruhi hayo wakati wa mechi ya ufunguzi wa ligi kuu nchini Uingereza kati ya Arsenal na Liverpool katika uwanja wa Emarates ambapo Liverpool ilishinda 4-3.

Kocha huyo amesema ni pigo kubwa kwa mchezaji huyo kukosa mechi hiyo ya kufuzu kombe la dunia kwani ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi chake.

Coleman: Akishangilia na mchezaji Ramsey kwenye mechi dhidi ya Urusi.
Coleman: Akishangilia na mchezaji Ramsey kwenye mechi dhidi ya Urusi.

Pia kocha huyo amemshtumu kocha Arsene Wenger kwa kumtumia mchezaji huyo kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu bila ya kumpa mapumziko baada ya kuitumikia Wales kwenye michuano ya Euro iliyofanyika nchini Ufaransa.

Coleman ameongeza kwa kusema kwamba alitarajia Wenger angempa mapumziko mchezaji huyo kama alivyofanya kwa baaddhi ya wachezaji kama  Mesut Ozil, Olivier Giroud na Laurent Koscielny.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *