Kiungo wa Wales na klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey atakosa mechi mbili za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Austria na Georgia kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya misuli.

Ramsey mwenye miaka 25 hakucheza mechi yoyote toka aumie kwenye mechi ya kwanza ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi nchini Uingereza dhidi ya Liverpool.

Wales wameanza harakati zao za kuwania kufuzu kombe la dunia kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Moldova ambayo wameshinda jumla ya goli 4-0.

Mechi inayofuata ya Wales itakuwa dhidi ya Austria itakayochezwa Oktoba 6 mwaka huu ikifuatiwa na Georgia siku tatu baadae itakayofanyika katika mji wa Cardiff.

Ramsey ni miongoni mwa wachezaji walioisadia wales kufika hatua ya nusu fainali katika michuano ya Euro iliyomalizika nchini Ufaransa ambapo walifungwa 2-0 dhidi ya Ureno kwenye hatua hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *