Muigizaji nyota wa Bongo movie, Rammy Galis amesema pengo aliloacha msanii wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba halitazibika kutokana na mchango wake kwenye filamu.

Muigizaji huyo amesema kuwa mchango wa Kanumba ni mkubwa sana na pengo lake litabakia kuwa hivyo na yeye amefanikiwa kufanya naye kazi mwishoni mwishoni kabla ya mauti kumkumba alikuwa ni mtu wa aina yake.

 

kanumba

Pia Galis amesema wasanii wa filamu nchini wanatakiwa kubadilika kulingana na matukio yanayofanyika katika jamii na kuepuka kufanya uigizaji wa zamani wa kuzunguka na magari na kukaa sebuleni kwenye makochi.

 

Pamoja na hayo Galis amesema mwezi Desemba mwaka huu anatarajia kuachia filamu aliyoigiza na waigizaji wa Nigeria na kuwataka wadau kukaa mkao wa kula kuburudika na kazi yake kwani imeandaliwa kwa viwango vya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *