Muigizaji nyota wa Bongo movie, Rammy Galis amefunguka kwa kusema kuwa watu wanaojihusisha na kundi la Freemason walimualika kujiunga na kundi hilo kwa njia ya simu yake ya mkononi.

Galis amesema yeye hajajiunga na Freemason na wala hatafanya hivyo lakini alishawahi kutumiwa ujumbe wa kujiunga lakini amekataa kufanya hivyo kutokana na imani yake kutoruhusu kufanya hivyo.

Galis alikuwa akijibu swali kutoka kwa mmoja ya mashabiki wake aliyetaka kujua iwapo Diamond pia yupo katika kundi la Freemason au illuminati kama ilivyokuwa ikidaiwa kwa marehemu Steven Kanumba, ambapo alisema kuwa yeye hawezi kufahamu, na kukiri kuwa suala hilo kwa wasanii lipo na ni la kawaida.

Kwa upande mwingine msanii huyo amesema anatarajia kuachia filamu mpya mwezi Desemba mwaka huu na kuwataka wananchi kumuunga mkono kwani itakuwa na ubora wa hali ya juu na kwamba ameitengenezea nje ya nchi na wasanii wakubwa wa Nigeria.

Vile vile Rammy Galis amewataka wasanii wa Bongo Movie kukaza katika soko la sasa na kuto kata tamaa kwani mafanikio hayaji bure bila kuweka juhudi za makusudi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *