Muigizaji wa Bongo Movies, Rammy Galis amesema kuwa amekuwa na furaha baada ya kupata nafasi ya kufanya filamu na waigizaji wakubwa barani Afrika, Aki na Ukwa.

Muigizaji huyo amesema filamu hiyo ambayo inaitwa ‘Welcome to Lagos’ itaanza kurekodiwa mwezi Disemba mwaka huu nchini Nigeria.

Ramy amesema hii itakuwa nafasi nzuri ya kuweka tasnia ya filamu nchini kwenye ramani ya kimataifa.

Muigizaji huyo ambaye hivi karibuni ameitambulisha filamu yake mpya ya ‘Red Flag’ iliyosimamiwa na watayarishaji kutoka Nollywood amesema filamu hiyo inahusu mahusiano na vioja vya kufurahisha.

Amesema kuwa  “Filamu inahusu mtu ambaye sio raia wa Nigeria ambaye anaenda Nigeria kwa Girlfriend wangu, kwa hiyo nafikia kwenye nyumba yake halafu Aki na Ukwa ni wadogo zake,”.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Kwa hiyo wanakuwa shemeji zangu, mimi nakuwa kama king’asti, sina hela, kwahiyo yule msichana akienda kazini nakuwa napambana na hao akina Aki na Ukwa ambao hawanipendi wananifanyia vituko,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *