Staa wa filamu za mapigano nchini Marekani, Sylvester Stallone maarufu kama Rambo amekata kufanya kazi chini ya Serikali ya Donald Trump itakayoingia madarakani Januari mwakani.

Taarifa zilizoenea wiki iliyopita zilikuwa zinasema kuwa Rambo amepewa nafasi kwenye Ofisi ya Serikali ya kutoka pesa kwa vijana wenye mawazo mazuri kwenye mambo ya sanaa Marekani ‘National Endowment for the Arts (NEA)‘.

Staa huyo ameasema kuwa amefurahi kusikia kuwa ametajwa kwaajili ya nafasi hiyo ila amekata sababu ana imani anaweza kufanya jambo zuri zaidi kwa wanajeshi wanaorudi nyumbani kwa sasa nchini Marekani kwa kuwatafutia kazi, sehemu ya kuishi na kuwapa nafasi ya kuwa pamoja na familia na jamii zao.

Rambo ni muigizaji mkongwe aliyejizolea umaarufu duniani kote kupitia filamu zake zilizofanya vizuri wakati wa kipindi chake alichokuwa anavuma.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *