Mkali wa RnB Bongo, Rama Dee ametumia akaunti yake ya Instagram kumpa ujumbe Director maarufu Bongo, Adam Juma kuwa ajipange ili kufikia ubora wa Hansacana kwasasa.

Kwenye ujumbe huo mwanamuziki huyo amemwambia Adam Juma kuwa anaweza kujifunza kutoka kwa Hanscana ili haweze kufikia levo za director huyo au kumpita zaidi.

Kutokana na ujumbe huo kwenye akaunti yake ya Instagram baadhi ya mashabiki wake wamemchana kwa kumwambia kuwa hana busara kwa kumfananisha Hanscana na Adam Juma.

Baada ya muda mfupi Adam Juma akajibu ‘post’ hiyo ya Rama Dee kwa kuweka picha ya Hanscana na kuandika kuwa ‘Wangejua jinsi tukoje wangelala tu’ Nakuheshimu wewe na kazi zako.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *