Rais wa zamani wa Korea Kusini kukamatwa

0
252

Aliyekuwa rais wa taifa Korea Kusini, Park Geun-hye uhenda akakamatwa kutokana na  kwa kashfa ya ulaji rushwa nchini humo.

Park Geun-hye amefuunguliwa mashtaka mapema mwezi huu na akaondolewa rasmi madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kudumisha uamuzi wa bunge wa kumng’oa madarakani.

Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwa kubwa nchini humo.

Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14.

Waendeshaji mashtaka wamesema kuwa wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata”.

Pia wamesema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ukaharibiwa iwapo Bi Park hatakamatwa.

Bi Choi anatuhumiwa kutumia uhusiano wake na rais huyo kushinikiza kampuni kutoa mamilioni ya dola kama mchango kwa nyakfu za kusaidia jamii ambazo alikuwa anazisimamia.

LEAVE A REPLY