Rais wa zamani wa Iran, Akbar Hashemi Rafsanjani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rafsanjani alikuwa akimuunga mkono rais wa sasa Hassan Rouhani ambae amemsifu kuwa ni mwana mapinduzi mkubwa.

Siku tatu za maombolezi zimetangazwa kwa kiongozi huyo aliyekuwa rais wa nne wa Serikali ya Iran kuanzia mwaka 1989 hadi 1997.

Ayatollah Rafsanjani aliwahi kuwa rais kati ya mwaka 1989 hadi 1997 na ameendelea kuwa na nafasi muhimu katika siasa za Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *