Rais wa shirikisho la soka la Ulaya (Uefa), Aleksander Ceferin amesema bado anafuatilia pendekezo lake la kutaka fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya ichezewe nje ya bara hilo.

Rais huyo amesema atafufua tena juhudi zake za kutaka miji iwe ikituma maombi ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo.

Amesema kuwa anaunga mkono fainali kuchezewa katika mji wa New York nchini Marekani miaka ya mbele.

Fainali zote 61 zilizochezwa awali zilichezewa Ulaya lakini Ceferin amesema haliwezi likawa tatizo kwa mashabiki wa soka kusafiri Marekani.

Cafferin amesema kuwa kusafiri kutoka Ureno hadi Azerbaijan kwa mfano ni karibu sawa au ni sawa na kwenda New York.

Kunaweza kuwa na tatizo la nyakati hata hivyo, ikizingatiwa mabadiliko ya saa katika mabara mbalimbali.

Mkuu huyo wa Uefa hata hivyo hana mipango ya kubadilisha wakati wa kuanza kwa fainali, ambayo kawaida huchezwa saa 19:45 BST (20:45 GM).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *