Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amerejea nchini mwake akitokea Uingereza alipokuwa anapatiwa matibabu ya Afya yake.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 74 ambaye aliwasili kupitia uwanja wa ndege wa kijeshi wa Kaduna nchini humo sasa yuko katika mji mkuu Abuja.

Kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi aliondoka nchini Nigeria tarehe 19 Januari na amekuwa akifanyiwa ukaguzi wa kimatibabu mjini London.

Maelezo ya afya yake hayajatolewa ,lakini kulingana na ujumbe wa Twitter kutoka kwa msaidizi wake Bashir Ahmed amesema kuwa rais amefurahia kurudi nchini humo.

Buhari alishukia katika uwanja wa ndege wa kaduna kwa kuwa uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Abuja umefungwa kwa muda ukifanyiwa ukarabati.

Likizo ya Buhari iliongezwa muda kutokana na ushari wa daktari wa kumfanyia vipimo zaidi na kumpumzisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *