Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi anatarajia kuwa rais wa kwanza wa Afrika kukutana na rais mpya wa Marekani, Donald Trump angu alipoapishwa mwezi Januari mwaka huu.

Rais huyo wa Misri yuko jijini Washington kwaajili ya kukutana na mwenyeji wake.

Rais al-Sisi pia alikuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kutuma salamu za pongezi kwa rais Donald Trump kufuatia ushindi wake dhidi ya Hillary Clinton kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa viongozi hao wanatarajiwa kujadiliana kuhusu mchakato wa kuleta amani baina ya Palestina na Israel pamoja na mapambano dhidi ya kundi la IS.

Viongozi hao waliwahi kukutana nchini Marekani mwezi Septemba jijini New York wakati Sisi alipokuwa akienda kuhudhuria mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *