Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais John Pombe Magufuli kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Amewasili kwa ndege maalum ya serikali ya Misri na kupokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ni ziara ya kwanza kwa rais wa huyo wa Misri nchini Tanzania ambapo ameongozana na msafara wake kwa ajili ya ziara hiyo ya siku mbili nchini Tanzania.

Wiki iliyopita mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwataka wakazi wa Dar es Salaam wenye Hotel, Magari na Migahawa kuchangamkia fursa ya ugeni huo katika kufanya biashara ili kujipatia kipato na kukuza Biashara zao.

Pia Makonda aliwataka wakazi wa Dar es salaam kuonyesha ukarimu tangu Rais atakapowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere hadi hapo atakaporejea nchini Misri siku ya Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *