Rais wa Gambia, Yahya Jammeh amesema kuwa atakwenda mahakamani kupinga ushindi wa rais mteule wa nchi hiyo Adama Barrow kutokana na udanganyifu kwenye uchaguzi.

Awali Rais Jammeh alikubali kushindwa baada ya mpinzani wake Adama Barrow kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa wiki iliyopita, lakini baadae alibadilisha kauli yake na kusema anakataa matokeo.

Mitaa ya mji mkuu Banjul iko katika hali ya utulivu huku jeshi likipiga doria mjini humo.

Muungano wa Jammeh -Alliance for Patriotic Reorientation and Construction party Ulitangaza usiku wa Jumamosi , kwamba utawasilisha kesi katika mahakama kuu ya Gambia.

Kwa mujibu wa sheria za Gambia, malalamiko kuhusu matokeo yanaweza kupingwa kisheria katika kipindi cha siku 10 baada ya kupigwa kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *