Rais wa Shirikisho la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino ametuma salamu za pongezi kwa timu ya Yanga baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/17.

Fifa imeipongeza Yanga baada ya kumaliza msimu ikiwa kileleni na pointi 68 ambazo ni sawa na za Simba, lakini Yanga imeweza kuwa bingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ambayo ni kumi.

Salamu za Fifa kwa Yanga zimewasilishwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi baada ya leo kuandika kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter.

Yanga walitwaa kombe la ligi kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfufululizo baada ya kufungana points na klabu ya Simba zote za jijini Dar es Salaam.

Licha ya salamu hizo za pongezi kwa Yanga, klabu ya Simba bado wanasikiliza rufaa yao waliyoikata dhidi ya beki wa Kagera Sugar Mohamed Fakhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *