Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA), Gianni Infantino amemtumia salamu za rambirambi rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kufuatia kifo cha Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan.

Rais Infantino, katika salamu zake kwa Rais Malinzi, alianza kwa kusema: “Tafadhali pokea salamu zangu za rambirambi baada ya kusikia kifo cha Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan ambaye ni mchezaji mwenye umri wa chini ya miaka 20.

Kifo cha mchezaji Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza kilitokea Desemba 4 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera wakati timu yake ikicheza mchezo huo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Ismail alianguka uwanjani dakika ya 74 alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.

Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa Kagera. Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alizikwa Desemba 5, 2016 jijini Mwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *