Rais wa shirikisho la Soka Afrika (CAF) Ahmed Ahmed amewasili mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kwa ziara maalum.

Rais huyo wa CAF anatarajiwa kuamuru kuondoshwa kwa vikosi vya Umoja wa Afrika vilivyopiga kambi kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu, atakapokutana na waziri mkuu wa Somalia Hassan Ali Kheyre baadaye leo.

Rais na ujumbe wake akiwemo mjumbe wa kamati kuu Souleiman Hassan Waberi na Mohamed Thabet walipokelewa kwenye Uwanja wa ndege na Rais wa Shirikisho la Soka Somalia, Abdiqani Said Arab.

Wakati wa ziara hiyo nchini Somalia, Rais wa CAF atatembelea viwanja vitatu vya mpira na atahutubia wachezaji wa taifa hilo ambao wako kambini wakijiandaa kupambana na Sudani kusini nchini Djibouti katika hatua ya awali ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika.

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika Ahmed Ahmed, amekuwa kiongozi wa juu wa kwanza kuwasili nchini Somalia na kuwasili kwake nchini humo kunatazamwa kuwa hatua ya kutia moyo kwa nchi hiyo inayopenda mchezo wa soka, ambayo kwa sasa inajitahidi kurejea katika hali yake baada ya miongo kadhaa ya vita na machafuko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *