Rais wa Marekani, Barack Obama amezungumzia sera dhidi ya ugaidi na kila kinachopaswa kufanyika katika siku za usoni katika vita dhidi ya ugaidi bila kuingiza masuala ya ubaguzi.

Ameyasema hayo katika hotuba yake ya mwisho kuhusiana na masuala ya usalama na kueleza kile kilicho fanyika katika utawala wake kuhusiana na usalama

Akizungumza katika kambi ya jeshi la anga ya MacDill ,Tampa, jimboni Florida,Rais Obama amesema kuwa vita dhidi ya ugaidi,haipaswi kupoteza mwelekeo wake na misingi iliyowekwa.

Obama amesisitiza kuwa Marekani si mahala ambapo raia anapaswa kutembea na kitambulisho mkononi kujihakikisha kuwa si adui.

Pia Obama amewapongeza wale aliowaita ,walisaidia kuifanya Marekani kuwa mahala salama katika utawala wake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *