Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy atasimamishwa kizimbani kujibu mashtaka ya kutumia njia haramu kutumia fedha kwaajili ya kampeni za siasa.

 Sarkozy anakabiliwa na tuhuma za chama chake kupotosha jina la akaunti ili kuficha 18m euros (TZS42bn) za kampeni ambazo zilitumika kwenye kampeni za mwaka 2012.

Hata hivyo Sarkozy ameendelea kushikilia msimamo wa kukanusha kuwa alikuwa anatambua juu ya matumizi yaliyopitiliza.

Sarkozy alishindwa kutetea kiti chake mwaka huo dhidi ya rais wa sasa, Francois Hollande, kisha Sarkozy akashindwa tena kutetea nafasi ya kuchaguliwa na chama chake kwaajili ya kuwania tena urais kwenye uchaguzi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *