Rais mpya wa Ghana kuapishwa leo

0
296

Rais mpya wa Ghana, Nana Akuffo-Addo anatarajiwa kuapishwa leo kushika wadhifa huo baada ya kumshinda aliyekuwa rais wa taifa hilo lenye demokrasia bora zaidi barani Afrika, John Dramani Mahama kwenye uchaguzi mkuu.

Nana Akufo-Addo, aliyekuwa wakati mmoja wakili wa haki za kibinadamu alimshinda kiongozi wa sasa anayekabidhi ofisi leo hii, John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Karibu viongozi 11 wa mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo, ambako hali ya usalama tayari imeimarishwa.

Baada ya kuapishwa kwake, viongozi wa Afrika watajadiliana jinsi ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia Yahya Jamme anakubali kuwa alishindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

LEAVE A REPLY