Rais mpya wa Gambia, Adama Barrow leo anatarajiwa kurudi nchini humo kwa ajili ya kuiongoza nchi hiyo akichukua nafasi ya kiongozi aliyeondoka Yahya Jammeh.

Barrow aliapishwa wiki iliyopita Senegal wakati viongozi wa kieneo walipokuwa wakimshawishi kiongozi aliyekuwepo ajiuzulu.

Rais Barrow atakaa katika makaazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.

Maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi watasalia Gambia wakati kukiwa na taarifa kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *