Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuharakisha mchakato wa kutayarisha Sera ya Diaspora itakayotumika kama mwongozo wa kushirikisha jamii ya Watanzania waishio nje ya nchi kuchangia kukuza uchumi.

Rais Magufuli amesema hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, wakati akifunga mkutano wa Diaspora mjini Unguja jana.

Amesema kuwepo kwa Sera ya Diaspora kutaifanya jamii hiyo kushiriki kuchangia maendeleo ya taifa katika uwekezaji hivyo kuinua uchumi.

Rais mesema malengo ya Serikali ni kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 katika sekta ya viwanda, uwekezaji, kilimo na utalii ili kukuza pato la Taifa.

Pia amesema anaagiza Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuharakisha mchakato wa kutayarisha Sera ya Diaspora ambayo itatoa nafasi kwa jamii kushiriki kuchangia kukuza uchumi na kuzalisha ajira kutokana na uwekezaji wao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *