Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tatu, Banjamin Wiliam Mkapa jana amesherehekea kumbu kumbu ya ndoa yake na mkewe Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbali mbali waliudhuria kwenye sherehe hiyo ambapo walipata chakula cha machana kwa pamoja.

Mazungumzo: Edward Lowassa akiteta jambo na katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa Sherehe ya rais mstaafu, Benjamin Mkapa jana jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo:Mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akiteta jambo na katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa Sherehe ya rais mstaafu, Benjamin Mkapa jana jijini Dar es Salaam.

Viongozi waliohudhuria kwenye sherehe hiyo maarufu kama Jibilei ya dhahabu ni pamoja na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Abdulrahman Kinana.

Pia Aliyekuwa Waziri Mkuu na mgombea urais kupitia CHADEMA, Edward Lowasaa nae alihudhuria kwenye sherehe hiyo ambapo alionekana mtu mwenye furaha alipokuwa anasalimiana na rais Magufuli pamoja na Kinana.

Viongozi hao walionekana wenye furaha kwa pamoja kwa kuacha tofauti zao kwenye siasa na kuungana kuwa kitu kimoja wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli na Lowasa walikuwa kwenye kinyanganyiro cha kugombea urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana ambapo Rais Magufuli ameshinda na kuwa rais wa awamu ya tano wa Tanzania huku Lowassa akipingana na matokeo hayo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi hapa nchini.

Lowassa kwasasa ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA ambapo nae ameshiriki katika mazungumzo ya kuanzishwa kwa maandamano ya Septemba mosi maarufu kama ‘UKUTA’  kupinga Serikali ya rais Magufuli.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *