Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wamesaini mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Ohima, Uganda hadi Tanga.

Magufuli amesema walikuwepo matapeli wengi wakati wa mchakato wa ujenzi wa bomba hilo na kuwa anafurahia zaidi kuingia mkataba huo na Uganda.

Rais Magufuli amesema kuwa “Nina furaha sana, najua Museveni anaijua Tanzania, anajua vichochoro vyote vya Ikulu na yeye ni zao la Mwalimu Nyerere.

Kwa upande wake Rais Museven amesema kuwa mkataba huo utaimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili za ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkataba huo umesainiwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo rais Museven alikuja nchini kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *