Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli wamesema wataifanyia mabadiliko Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) kutokana na kushindwa kujiendesha kibiashara.

Marais hao walilijadili kwa kina na kubaini kuwa tatizo ambalo limechangia kufifisha uwezo wa shirika hilo ni menejimenti, hivyo wameahidi kufanya mabadiliko makubwa katika eneo hilo.

Katika mabadiliko hayo, viongozi hao wamekubaliana kubadilisha kwanza sheria zinazoendesha shirika hilo ambalo lilianzishwa mwaka 1976 ili ziruhusu ajira ya mkurugenzi mkuu na wasaidizi wake watoke nchi yoyote duniani kutokana na uwezo wao wa kazi. Sheria ya sasa ya Tazara inasisitiza kuwa mkurugenzi mkuu lazima aajiriwe kutoka Zambia na msaidizi wake lazima awe Mtanzania.

Kwa mujibu wa viongozi hao wawili, katika mazungumzo yao wamekubaliana kwamba wanasheria wakuu wa nchi hizo wakutane waone namna ya kubadilisha sheria hiyo.

Usafirishaji wa shehena unaofanywa na Tazara umeshuka kutoka kusafirisha tani milioni 5 kwa mwaka hadi kufikia tani 128,000. Kwa upande wake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *