Rais wa Jamhuri ya Muunga wa Tanzania, Dkt John Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili za Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) zilizonunuliwa kwa kutumia kodi za wananchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anaeshughulika na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1).

Dkt. Chamuriho amesema ndege ya kwanza iliwasili nchini Septemba 20 na ndege ya pili ilitarajiwa kuwasili nchini leo saa 6:00 mchana.

Katibu Mkuu huyo pia amesema ndege hizo zimenunuliwa na Serikali ili kuhudumia wananchi wa ndani na nje ya Tanzania.

Pia amesema kuwa “Ndege hizo aina ya Dash 8 Q400 zimetengenezwa na kiwanda cha Bombadier nchini Canada ambapo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 76 na zitatumika katika kuhudumia soko la ndaniya Tanzania na nchi jirani,”.

Vile vile Dkt Chambuso amesema Serikali ya Tanzania inawakaribisha wananchi wote kushuhudia uzinduzi wa ndege hizo unaotarajiwa kuanza saa mbili kamili asubuhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *