Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kuwa anaisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanavyeti feki vya kufoji ili aifanyie kazi.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akizindua majengo ya Hostel za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).

Pia Rais Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo.

Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua aina ya vyuo ambavyo wao wanataka kwenda.

Kutokana na na hayo kutatoa nafasi kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia wakienda kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *