Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajia kuanza ziara nchini Kenya.

Ziara ya Magufuli nchini humo inakuja wakati ambapo uhusiano wa mataifa hayo mawili umekuwa ukilegea kwa siku za karibuni.

Kwenye ajenda ya ziara hiyo rasmi ya kiserikali kati yake na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, ni kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.

Tangu aingie madaraka mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli amezuru mataifa mawili ya Rwanda na Uganda

Pia ziara ya Dkt Magufuli inahusu na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kumpendekeza waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya, Amina Mohammed kwa kinyanganyiro cha wadhifa wa mwenyekiti wa muungano wa afrika-AU.

Rais Uhuru Kenyatta atamkaribisha mgeni wake jijini Nairobi, baada ya Kenyatta kukamilisha ziara ya siku mbili huko Khartoum, alipokutana na Rais wa Sudan- Omar Al- Bashir.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *