Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezitaka mahakama kukusanya shilingi tilioni 7.3 ambazo ni matokeo ya Serikali kushinda kesi mbali mbali za ukwepaji kodi.

Rais Magufuli ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Magufuli amesema kuwa takwimu zilikuwa zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi pingamizi za kodi ambazo serikali imeshinda kesi hizo japokuwa fedha hizo hazijakusanywa kwasasa.

Pia Rais Magufuli amesema kuwa katika kuelekea kukua kwa uchumi mahakama iwe chanzo cha pato la taifa kuhakikisha wale wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo.

Kwa upande wake Kaimu Jaji mkuu, Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *