Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindua mabweni mapya ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Chuo Kikuu na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam, Paul Makonda pamoja na waziri wa Elimua, Profesa Joyce Ndarichako.

Katika hotuba yake kwenye uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuleta maendeleo katika sekta ya Elimu na kutatua changamoto za makazi kwa wanafunzi wa chuo.

Pia Rais Magufuli amepunguza gharama ya kuishi katika mabweni hayo kutoka shilingi mia nane hadi mia tano kwa siku.

Mabweni ya Chuo Kikuu (UDSM) yaliyozinduliwa na Rais Magufuli leo
Mabweni ya Chuo Kikuu (UDSM) yaliyozinduliwa na Rais Magufuli leo

Kwa upande mwingine Rais Magufuli ameutaka uongozi wa chuo hiko kuhakikisha wanakuwa na mabasi ya cho ili kukabiliana na usafiri kwa wanafunzi wanaotoka hosteli za Mabibo.

Mwisho Rais Magufuli amewataka wanafunzi wa chuo hiko kuhakikisha wanayatunzi mabweni hayo ili kuweza kutumika na wanafunzi wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *