Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo amezindua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.

Rais Magufuli ameupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya kutaka Tanzania ya viwanda kwa kujenga viwanda vingi mkoani humo ikiwa ni pamoja na viwanda hivyo viwili alivyovizindua katika siku yake ya mwisho ya ziara mkoani Shinyanga.

 

Pia ameitaka Benki ya Uwekezaji Nchini TIB na Taasisi nyingine za fedha kutoa mikopo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika viwanda badala ya kuwakopesha wanasiasa ambao hutumia fedha wanazokopa kwa matumizi yasiyowanufaisha watanzania waliowengi.

 

Rais Magufuli yupo ziarani mikoa ya kanda ya ziwa ambapo jana alisheherekea sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *