Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amezindua barabara ya KIA mpaka Mererani mkoani Manyara.

Baada ya kuzindua barabara hiyo Rais Magufuli  amewashukuru wizara ya ujenzi na uchukuzi, TANROADS, wakandarasi na consultants ambao wamefanikiwa kumaliza barabara hiyo ya KM 26 kwa gharama ya bilioni 32.5 na fedha zote zimetokana na kodi za watanzania.

Rais Magufuli amesema kuwa barabara ambazo tumeamua kutengeneza zipo yingi, tumeanza na Km 26 lakini haiwezi kuishia hapa kabla haijafika makao makuu ya wilaya na Mkoa.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amezungumzia suala la madini ya Tanzanite ambayo inachimbwa maeneo ya Mererani mkoani Manyara.

Rais Magufuli amesema kuwa ripoi ya Tanzanite iliyoundwa na Spika, Tanzania haiwanufaishi hata wananchi wa hapa, pia haiwanufaishi watanazania. Tanzania inapata asilimia tano, ndio maana nasema nasema tuna changamoto.

Pia amesema kuwa kuna wawekezaji ambao wana asilimia 50 lakini mali zinasombwa sana na watanzania hawanufaiki kutokana na madini hayo.

Vile vile rais Magufuli amesema kuwa ili tuzuie wizi, block A mpaka D ameagiza JWTZ waanze kulijenga ukuta eneo lote, kazi ifanyike haraka na waweke fence na kamera ili kubaini wezi wa madini hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *