Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kuwa sababu ya kuvunja bodi ya mamlaka ya mapato TRA kutokana na mamlaka hiyo kuweka mabilioni ya fedha katika benki binafsi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika sherehe ya mahafali ya Chuo Kikuu Huria  Kibaha Mkoa wa  Pwani.

Pia Rais amesema kwamba TRA walichukua mabilioni ya  fedha na kuyaweka kwenye akaunti za muda maalum (fixed accounts) katika  benki nane ambapo bodi ikaidhinisha.

Wiki iliyopita Rais Magufuli alivunja bodi hiyo na kutengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu bila kueleza sababu zozote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *