Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amewatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold.

Wajumbe hao ni wale walioshiriki katika kamati alizounda Rais Magufuli kuhusu uchunguzi wa mchanga wa madini (Makinikia).

Katika hatua nyingine Rais Magufuli, amemteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, baada ya aliyepo sasa, Gavana Benno Ndulu kumaliza muda wake.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiunuku vyeti kwa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia, ikulu jijini Dar es Salaam.

Luoga ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikuwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uteuzi wake utaanza baada ya Benno Ndulu kumaliza muda wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *