Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo ametembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwaona wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo akiwemo mkewe Mama Janeth Magufuli.

Pia Rais Magufuli ametembelea hospitalini hapo kutoa pongezi kwa wauguzi kutokana na kazi nzuri wanazozifanya.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli amezungumza na baadhi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kuhusu huduma wanayopata kutoka kwa madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo ya Taifa nchini.

Vile vile Rais Magufuli akusita kuwapa pongezi wauaguzi katika hospitali hiyo kwa kusema wanafanya kazi nzuri mpaka wagonjwa wanafurahia huduma wanayopata hospitalini hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *