Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewaomba watanzania kuwa wamoja ili kuijenga na kuiendeleza Tanzania.

 Rais amesema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari katika kutimiza mwaka mmoja tangu aanze kuiongoza Tanzania tangu uchaguzi mkuu mwaka jana.

Rais Maguguli amesema hakuchaguliwa ili kuongoza watu wachache bali kuwatumikia watanzania wote.

Vile vile Magufuli amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii ili wapate kipato kutokana na kazi wanazofanya.

Katika hatua nyingine Magufuli amesema siku akiletewa Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari atausaini muda huo huo ili uanze kufanya kazi mara moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *